Tanga (mji)
Jiji la Tanga
|
Jiji la Tanga
Mahali pa mji wa Tanga
katika Tanzania
|
historia ya Tanga (ca
1906)
Mji wa Tanga ni mji mkuu wa Mkoa wa Tanga uliyoko ufukoni mwa Bahari ya Hindi. Tanga ina bandari kubwa kabisa katika sehumu ya
kaskazini mwa Tanzania. Njia ya reli kwenda Mji wa Moshi inaanza hapa.
Jina hili la mji wa Tanga lilitokana
neno la Kiajemi lenye maana nne tofauti ambazo
ni: Iliyo nyooka; Bonde lenye rutuba; Barabara upande wa mto na Shamba juu ya
mlima, neno hilohilo la Tanga kwa kabila la Kibondei ambalo ni
wenyeji wa mkoa huo linamaana ya shamba, wao hulitamka N'tanga
Historia
Tanga insaemekana imeanzishwa na wafanyabiashara Waajemi katika karne ya 14 BK. Mji wa Tanga haikupata umuhimu kama
mji wa jirani ya Mombasa. Tarihi
ya Pate inasema
ya kwamba kabla ya kuja kwa Wareno Pateiliwahi kutawala Lindi kwa muda fulani.
Katika karne ya 19 BK Tanga ilikuwa chini ya utawala wa Omani na Zanzibar. Misafara ya biashara imeanzishwa hapa kwenda bara.
Kutokana na bandari yake nzuri ya kiasili Tanga ilikua sana wakati wa ukoloni
wa Wajerumani waliojenga bandari wa kisasa pamoja reli kwanda Moshi. Reli iliwezesha kilimo kwa ajili ya
soko la dunia Tanga ikawa bandari kuu kwa jili ya katani na kahawa. Baada ya Uingereza
kuchukua utawala wa Afrika
ya Mashariki ya Kijerumani reli ya Tanga-Moshi iliunganishwa na ile ya kati
hivyo ikawa na njia kwenda Daressalaam pia. Wakati waVita
Kuu ya Kwanza ya Dunia Tanga iliona mapigano makali tar. 3 - 5 Novemba 1914. Jaribio la Uingereza kuvamia Tanga kwa kikosi cha maaskari 8000 Waingereza na Wahindi kutoka meli kwenye Bahari Hindi ilishindwa vibaya naJeshi la Ulinzi wa Kijerumani chini ya uongozi wa Paul von Lettow-Vorbeck.
Mwaka 1922 "Tanganyika Territory African Civil Services Association" (TAA) iliundwa Tanga ambayo
ilikuwa shirika ya kwanza ya Kiafrika yenye shabaha za kisiasa.
Kutokana na kupanuka kwa bandari ya Daressalaam umuhimu
wa bandari ya Tanga umerudi nyuma.
No comments:
Post a Comment